Al-Kahf 18:72
الكهفقَالَ أَلَمْ أَقُلْ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِىَ صَبْرًا
Akasema: Je, sikusema kwamba wewe hakika hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Sikukwambia hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami? [72]
[72] Yule mja mwema akasema: Mimi nilikwisha kwambia kuwa hakika wewe hutoweza kusubiri kuwa nami.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Al-Khiḍr akamwambia, «Nilisema tangu mwanzo, Hakika wewe hutoweza kuvumilia kufuatana na mimi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net