Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 56

Al-Kahf 18:56

الكهف

وَمَا نُرْسِلُ ٱلْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ ۚ وَيُجَـٰدِلُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِٱلْبَـٰطِلِ لِيُدْحِضُوا۟ بِهِ ٱلْحَقَّ ۖ وَٱتَّخَذُوٓا۟ ءَايَـٰتِى وَمَآ أُنذِرُوا۟ هُزُوًا

Maana

Na hatuwatumi Mitume isipokuwa wawe wabashiri na waonyaji. Na wale waliokufuru wanabishana kwa batili, ili kwayo waivunje haki. Na walizifanya Ishara zangu na yale waliyoonywa kuwa ni mzaha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hatuwatumi Mitume ila wawe wabashiri na waonyaji. Na walio kufuru wanabishana kwa uwongo, ili kwa uwongo huo waivunje kweli. Na wanazifanya Ishara zangu na yale waliyo onywa kuwa ni mzaha. [56]

[56] Lakini Mwenyezi Mungu hawatumi Mitume wake ila kwa ajili ya kutoa bishara njema na kuonya. Wala hawatumi kwa ajili ya hao wenye inda wawatake walete muujiza makhsusi. Lakini walio kufuru wanaacha hoja, na wanabishana na Mitume kwa upotovu ili waipotoe Haki. Na msimamo wao kwa Qur'ani na maonyo ni msimamo wa mwenye kejeli na maskhara ambaye hana makusudio ya kutafuta hakika ya mambo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hatuwatumi Mitume kwa watu isipokuwa wawe ni wenye kuwabashiria Pepo wenye Imani na matendo mema na kuwaonya na Moto wenye kukanusha na kuasi. Na pamoja na kuwa haki iko wazi ila wale waliokanusha wanagombana na mitume wao kiubatili kwa njia ya upotofu, ili wapate kuiondoa, kwa ubatilifu wao, haki aliyokuja nayo Mtume, na wamekifanya kitabu changu, hoja zangu na adhabu ambayo walionywa nayo kuwa ni shere na ni kitu cha kufanyiwa mzaha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net