Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 55

Al-Kahf 18:55

الكهف

وَمَا مَنَعَ ٱلنَّاسَ أَن يُؤْمِنُوٓا۟ إِذْ جَآءَهُمُ ٱلْهُدَىٰ وَيَسْتَغْفِرُوا۟ رَبَّهُمْ إِلَّآ أَن تَأْتِيَهُمْ سُنَّةُ ٱلْأَوَّلِينَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ ٱلْعَذَابُ قُبُلًا

Maana

Na hakikuwazuia watu kuamini ulipowajia uongofu, na kuomba maghfira kwa Mola wao Mlezi, isipokuwa iwafikie desturi ya wale wa mwanzo, au iwafikie adhabu jahara.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hapana kilicho wazuia watu kuamini ulipo wajia uwongofu na wakaomba maghfira kwa Mola wao Mlezi, isipo kuwa yawafikie ya wale wa zamani, au iwafikie adhabu jahara. [55]

[55] Na hapana lililo wazuia washirikina kuamini zilipo wafikia sababu za kuongoka, nazo ni huyu Mtume na Qur'ani, isipo kuwa ukaidi wao na kumtaka Mtume awaletee aliyo waletea Mwenyezi Mungu wale watu wa zamani, nayo ni kuangamizwa moja kwa moja kama kulio wapata hao wa kale, au awaletee adhabu ya dhaahiri hivi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hakuna kilichowazuia watu kuamini, alipowajia Mtume Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, akiwa na Qur’ani, na kumuomba maghufira Mola wao kwa kutaka Awasamehe, isipokuwa ni kule kushindana kwao na Mtume, kutaka kwao wajiwe na mwendo wa Allah Mtukufu wa kuwaangamiza watu waliopita kabla yao au wapatwe na adhabu ya Allah Mtukufu waziwazi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net