Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 54

Al-Kahf 18:54

الكهف

وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِى هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانِ لِلنَّاسِ مِن كُلِّ مَثَلٍ ۚ وَكَانَ ٱلْإِنسَـٰنُ أَكْثَرَ شَىْءٍ جَدَلًا

Maana

Na bila ya shaka tumewaelezea watu katika Qur-ani hii kila namna ya mfano. Lakini mwanadamu amezidi kuliko kila kitu kwa ubishi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na bila ya shaka tumewaelezea watu katika hii Qur'ani kila namna ya mfano. Lakini mwanaadamu amezidi kuliko kila kitu kwa ubishi. [54]

[54] Na Mwenyezi Mungu amewatajia watu katika Qur'ani hii, wanayo ikanusha na wakataka waletewe muujiza mwenginewe, mifano namna kwa namna, ili wapate kuwaidhika kwayo. Lakini mwanaadamu tabia yake ni kupenda kubishana. Akiwa kafiri basi atabisha hata kwa uwongo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika tumeeleza na kufafanua katika hii Qur’ani aina nyingi ya mifano ili wawaidhike na waamini. Na mwanadamu ni mwingi wa utesi na ubishi miongoni mwa viumbe.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net