Al-Kahf 18:57
الكهفوَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِـَٔايَـٰتِ رَبِّهِۦ فَأَعْرَضَ عَنْهَا وَنَسِىَ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ ۚ إِنَّا جَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِىٓ ءَاذَانِهِمْ وَقْرًا ۖ وَإِن تَدْعُهُمْ إِلَى ٱلْهُدَىٰ فَلَن يَهْتَدُوٓا۟ إِذًا أَبَدًا
Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Ishara za Mola wake Mlezi, naye akazipuuza na akasahau yaliyotangulizwa na mikono yake? Hakika Sisi tumeziba nyoyo zao ili wasifahamu, na uziwi uko kwenye masikio yao. Na ukiwaita kwenye uongofu, kamwe hawataweza kuongoka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ni nani dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye kumbushwa Ishara za Mola wake Mlezi, naye akazipuuza na akasahau yaliyo tangulizwa na mikono yake? Hakika Sisi tumeweka vifuniko juu ya nyoyo zao ili wasifahamu, na uziwi kwenye masikio yao. Na ukiwaita kwenye uwongofu hawakubali kabisa kuongoka. [57]
[57] Na hapana yeyote aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko huyo anaye waidhiwa kwa Ishara za Mola wake Mlezi naye asizingatie, na akasahau nini matokeo ya maasi yake anayo yatenda! Hakika Sisi kwa sababu ya kuelekea kwao kwenye ukafiri tumeweka vifuniko juu ya nyoyo zao, basi nyoyo zao hazitambui wala haziingii mwangaza. Na masikioni mwao tumetia uziwi basi hawasikii la kuwafahamisha! Nawe, ewe Mtume! Ukiwaita kwenye Dini ya Haki hawato ongoka maadamu tabia yao ni hii.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hakuna yoyote aliye mwingi wa udhalimu kuliko yule aliyepewa mawaidha ya aya za Mola wake zilizo wazi akazipuuza na akaendelea kwenye ubatilifu wake na akasahau matendo mabaya yaliyotangulizwa na mikono yake miwili asirudi nyuma. Sisi tumeweka vifuniko juu ya nyoyo zao ndipo wasiifahamu Qur’ani na wasiufikie wema uliyomo, na tumefanya ndani ya masikio yao kitu kinachofanana na uziwi ndipo wasiisikie na wasinufaike nayo, na ukiwaita kwenye Imani hawatakuitika na hawataongoka kuifuata kabisa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net