Al-Kahf 18:58
الكهفوَرَبُّكَ ٱلْغَفُورُ ذُو ٱلرَّحْمَةِ ۖ لَوْ يُؤَاخِذُهُم بِمَا كَسَبُوا۟ لَعَجَّلَ لَهُمُ ٱلْعَذَابَ ۚ بَل لَّهُم مَّوْعِدٌ لَّن يَجِدُوا۟ مِن دُونِهِۦ مَوْئِلًا
Na Mola wako Mlezi ni Msamehevu, Mwenye rehema. Lau angeliwachukulia kwa mujibu wa yale waliyoyachuma, bila ya shaka angeliwafanyia haraka kuwaadhibu. Lakini wanayo miadi ambayo hawatapata makimbilio yoyote ya kuepukana nayo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mola wako Mlezi ni Msamehevu Mwenye rehema. Lau angeli wachukulia kwa mujibu waliyo yachuma, bila ya shaka angeli wafanyia haraka kuwaadhibu. Lakini wanayo miadi ambayo hawatapata makimbilio yoyote ya kuepukana nayo. [58]
[58] Na Mola wako Mlezi Mtukufu Mwingi wa kusamehe makosa ya waja wake, Mwenye rehema kunjufu kwa mwenye kumuelekea, lau angeli penda kuwatwaa kwa maovu wayatendayo basi angeli wapatiliza upesi upesi kama alivyo kwisha watangulizia wenginewe. Lakini hii ni hikima yake aliyo ikadiria. Anawaakhirisha mpaka ufike wakati atapo waonjesha adhabu kali kabisa. Na hapo hawatopata pa kukimbilia na kuwalinda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Mola wako Ndiye Mwenye kusamehe dhambi za waja Wake wanapotubia, Ndiye Mwenye kuwarehemu. Lau angewatesa hawa wenye kuzipa mgongo aya Zake kwa madhambi na makosa waliyoyatenda, Angaliwaharakishia adhabu, lakini Yeye, Aliyetukuka, ni Mpole, Haharakishi kutesa. Lakini wana kipindi walichowekewa cha wao kulipwa kwa matendo yao, hawana njia ya kuepukana nacho wala kuhepa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net