Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 59

Al-Kahf 18:59

الكهف

وَتِلْكَ ٱلْقُرَىٰٓ أَهْلَكْنَـٰهُمْ لَمَّا ظَلَمُوا۟ وَجَعَلْنَا لِمَهْلِكِهِم مَّوْعِدًا

Maana

Na miji hiyo tuliwaangamiza watu wake walipodhulumu. Na tukawawekea miadi ya maangamizo yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na miji hiyo tuliwaangamiza watu wake walipo dhulumu. Na tukawawekea miadi ya maangamizo yao. [59]

[59] Na hii basi ndio miji ya kale tuliyo iteketeza pale watu wao walipo dhulumu kwa kuwakanusha Mitume wao. Na Sisi tukawawekea miadi ya kuwaangamiza isiyo na khitilafu. Hali kadhaalika itakuwa ya hao katika kaumu yako wanao kanusha, ikiwa hawaamini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Vijiji hivyo vilivyo karibu na nyinyi, kama vijiji vya watu wa Nûh, Sãlih, Lût, na Shu‛ayb, tuliviangamiza watu wake walipodhulumu kwa kukufuru, na tuliwawekea wakati na muda maalumu wa kuwaangamiza; walipoufikia adhabu iliwajia na Allah Mtukufu Akawaangamiza kwayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net