Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 60

Al-Kahf 18:60

الكهف

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِفَتَىٰهُ لَآ أَبْرَحُ حَتَّىٰٓ أَبْلُغَ مَجْمَعَ ٱلْبَحْرَيْنِ أَوْ أَمْضِىَ حُقُبًا

Maana

Na pale Musa alipomwambia kijana wake, "Sitaacha kuendelea mpaka nifike zinapokutana bahari mbili, au nitaendelea kwa muda mrefu."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na pale Musa alipo mwambia kijana wake: Sitoacha kuendelea mpaka nifike zinapo kutana bahari mbili, au nitaendelea kwa muda mrefu. [60]

[60] Na hakika hapana mtu anaye jua ya Mwenyezi Mungu ila Yeye Mwenyewe anapo mpa kipawa hicho Nabii au mtu mwema. Ewe Mtume! Simulia kuwa Musa bin Amran alimwambia kijana wake, mtumishi wake, mwanafunzi wake: Sitoacha kwenda mpaka nifike zinapo kutana bahari mbili, au basi nitaendelea kwenda tu muda mrefu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka pindi Mûsã alipomwambia mtumishi wake, Yûsha‛ bin Nûn, «Sitaacha kuendelea kutembea mpaka nifike kwenye makutaniko ya bahari mbili au niende kipindi kirefu mpaka nifike kwa mja mwema nipate kujifunza kwake elimu nisiokuwa nayo».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net