Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 61

Al-Kahf 18:61

الكهف

فَلَمَّا بَلَغَا مَجْمَعَ بَيْنِهِمَا نَسِيَا حُوتَهُمَا فَٱتَّخَذَ سَبِيلَهُۥ فِى ٱلْبَحْرِ سَرَبًا

Maana

Basi wawili hao walipofika zinapokutana hizo bahari mbili, walimsahau samaki wao, naye akashika njia yake akaponyokea baharini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi wawili hao walipo fika zinapo kutana hizo bahari mbili walimsahau samaki wao, naye akashika njia yake kaporonyokea baharini. [61]

[61] Basi Musa na kijana wake walipo fikilia pahala panapo kusanyika bahari mbili wakamsahau samaki wao walio kuwa wamemchukua kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Akatumbukia baharini, akashika njia yake katika maji!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakajibidiisha kwenda, na walipofika kwenye makutano ya bahari mbili walikaa penye jiwe la manga, na wakamsahau samaki wao ambaye Mûsã aliamuru achukuliwe kiwe ni chakula chao. Yûsha‛ alimbeba kikapuni, kutahamaki amekua hai na akawa anajivingirisha kuingia baharini, na akajifanyia njia iliyo wazi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net