Al-Kahf 18:62
الكهففَلَمَّا جَاوَزَا قَالَ لِفَتَىٰهُ ءَاتِنَا غَدَآءَنَا لَقَدْ لَقِينَا مِن سَفَرِنَا هَـٰذَا نَصَبًا
Walipokwishapita, alimwambia kijana wake: Tupe chakula chetu cha mchana. Kwa hakika tumepata machovu kweli kwa hii safari yetu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Walipo kwisha pita alimwambia kijana wake: Tupe chakula chetu cha mchana. Kwa hakika tumepata machofu kweli kwa hii safari yetu. [62]
[62] Musa na kijana wake walipo fika mbali na pahala pale, na wakaona njaa na machofu Musa akamwambia kijana wake: Tupe cha kukila. Hakika tumepata taabu na mashaka katika safari yetu hii.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Walipoondoka pale mahali walipomsahau samaki, na Mûsã akahisi njaa, alimwambia mtumishi wake, «tuletee chakula chetu cha mwanzo wa mchana, hakika tumechoka kwenye safari yetu hii».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net