Al-Kahf 18:63
الكهفقَالَ أَرَءَيْتَ إِذْ أَوَيْنَآ إِلَى ٱلصَّخْرَةِ فَإِنِّى نَسِيتُ ٱلْحُوتَ وَمَآ أَنسَىٰنِيهُ إِلَّا ٱلشَّيْطَـٰنُ أَنْ أَذْكُرَهُۥ ۚ وَٱتَّخَذَ سَبِيلَهُۥ فِى ٱلْبَحْرِ عَجَبًا
Akasema (kijana): Unaona! Pale tulipopumzika penye jabali, basi mimi nilimsahau yule samaki. Na hakuna aliyenisahaulisha kumkumbuka isipokuwa Shetani tu. Naye akashika njia yake baharini kwa ajabu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema (kijana): Waona! Pale tulipo pumzika penye jabali basi mimi nilimsahau yule samaki. Na hapana aliye nisahaulisha nisimkumbuke ila Shet'ani tu. Naye akashika njia yake baharini kwa ajabu. [63]
[63] Kijana wake akasema: Unakumbuka? Pale tulipo pumzika kwenye lile jabali, basi mimi nilimsahau yule samaki. Na hapana aliye nisahaulisha ila Shetani. Na hapana shaka samaki yule katumbukia baharini. Na mimi hakika najistaajabia kusahau kwangu huku.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mtumishi wake akamwambia, Unakumbuka tuliposhukia kwenye jiwe ambapo tulipumzika? Nilisahau kukwambia habari ya yule samaki, na hakuna aliyenisahaulisha isipokuwa ni Shetani. Na yule samaki, aliyekuwa amekufa, uhai umemrudia, akajirusha baharini na akajitolea njia ya kwendea, na mambo yake ni yenye kustaajabiwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net