Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 64

Al-Kahf 18:64

الكهف

قَالَ ذَٰلِكَ مَا كُنَّا نَبْغِ ۚ فَٱرْتَدَّا عَلَىٰٓ ءَاثَارِهِمَا قَصَصًا

Maana

(Musa) akasema: "Hayo ndiyo tuliyokuwa tunayataka." Basi wakarudi nyuma kwa kufuata njia waliyojia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

(Musa) akasema: Hayo ndiyo tuliyo kuwa tunayataka. Basi wakarudi nyuma kwa kufuata njia waliyo jia. [64]

[64] Musa akamwambia: Haya yaliyo tokea ndiyo tuliyo kuwa tunayataka kwa mujibu wa hikima anayo itaka Mwenyezi Mungu. Basi wakarejea nyuma kwa njia yao ile ile waliyo jia, wakizifuata nyayo zao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mûsã akasema, «Yaliyotokea ndiyo ambayo tulikuwa tukiyataka, kwani hiyo ni alama yangu ya mahali pa mja mwema.» Hapo wakarudi wakizifuata alama za nyayo zao mpaka wakakoma kwenye jiwe.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net