Al-Kahf 18:65
الكهففَوَجَدَا عَبْدًا مِّنْ عِبَادِنَآ ءَاتَيْنَـٰهُ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَعَلَّمْنَـٰهُ مِن لَّدُنَّا عِلْمًا
Basi wakamkuta mja katika waja wetu tuliyempa rehema kutoka kwetu, na tukamfunza mafunzo yaliyotoka kwetu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi wakamkuta mja katika waja wangu tuliye mpa rehema kutoka kwetu, na tukamfunza mafunzo yaliyo toka kwetu. [65]
[65] Mpaka wakafika kwenye lile jabali. Hapo wakamkuta mja miongoni mwa waja wangu walio wema, tuliye mpa hikima, na tukampa ujuzi mwingi kutokana kwetu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakamkuta mja mwema miongoni mwa waja wetu ambaye ni al-Khaḓir, amani imshukie- naye ni Nabii, miongono mwa Manabii wa Allah Mtukufu, ambaye Allah Mtukufu Amemfisha, tuliyempa rehema kutoka kwetu na tukamfundisha elimu kubwa itokayo kwetu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net