Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 66

Al-Kahf 18:66

الكهف

قَالَ لَهُۥ مُوسَىٰ هَلْ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰٓ أَن تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمْتَ رُشْدًا

Maana

Musa akamwambia: Nikufuate ili unifunze katika ule uongofu uliofunzwa wewe?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Musa akamwambia: Nikufuate ili unifunze katika ule uwongofu ulio funzwa wewe? [66]

[66] Musa akamwambia yule mja mwema: Je nende nawe upate kunifunza nami aliyo kufunza Mwenyezi Mungu?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mûsã akamsalimia na akamwambia, «Je, utaniruhusu nikufuate, unifundishe elimu ambayo Allah Mtukufu Amekufudisha kadiri ya mimi kujiongoza nayo na kunufaika?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net