Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 83

Al-Israa 17:83

الإسراء

وَإِذَآ أَنْعَمْنَا عَلَى ٱلْإِنسَـٰنِ أَعْرَضَ وَنَـَٔا بِجَانِبِهِۦ ۖ وَإِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ كَانَ يَـُٔوسًا

Maana

Na tunapomneemesha mtu, hugeuka na kujitenga kando. Na yanapomgusa maovu, hukata tamaa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mwanaadamu tunapo mneemesha hugeuka na kujitenga kando. Na inapo mgusa shari hukata tamaa. [83]

[83] Na hakika katika maumbile ya mwanaadamu ni kujidanganya na kukata tamaa. Tukimneemesha kwa kumpa uzima na ukunjufu wa mali, hupuuza kutukumbuka na kutuomba, na hujitenga nasi kwa kiburi na majivuno! Na akiguswa na shari, kama ugonjwa na ufakiri, huwa mwingi wa kukata tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tunapompa mwanadamu, vile alivyo, neema ya mali na afya na mfano wa hizo, anageuka na kujiweka mbali na kumtii Allah Mtukufu, na akipatikana na shida ya ufukara au ugonjwa huwa ni mwenye kukata tamaa, kwa kuwa yeye haamini kuwa atapata nyongeza njema za Allah Mtukufu Aliyetukuka, isipokuwa yule ambaye Allah Mtukufu Amemhifadhi katika hali yake ya raha na ya shida.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net