Al-Israa 17:84
الإسراءقُلْ كُلٌّ يَعْمَلُ عَلَىٰ شَاكِلَتِهِۦ فَرَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَنْ هُوَ أَهْدَىٰ سَبِيلًا
Sema, "Kila mmoja anafanya kwa namna yake. Na Mola wenu Mlezi ndiye anayejua zaidi yule aliyeongoka katika njia."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mwanaadamu tunapo mneemesha hugeuka na kujitenga kando. Na inapo mgusa shari hukata tamaa. [84]
[84] Ewe Nabii! Waambie makafiri wa Kikureshi kwa kuepuka kuchochea ugomvi na makindano: Kila mmoja wetu na mmoja wenu anatenda na anakwenda kwa kufuata njia yake. Na Mola wenu Mlezi ni Mjuzi mno, wala hana ajuaye kuliko Yeye kumjua nani aliye shika njia sawa na kufuata Haki. Na huyo humlipa ujira wake kaamili. Na kumjua aliye potea njia, na huyo humpa adhabu kama anayo stahiki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia watu, «Kila mmoja miongoni mwenu anatenda kulingana na hali zinazonasibiana na yeye, na Mola wenu ni Mjuzi zaidi wa yule aliyeongoka zaidi njia ya haki».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net