Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 85

Al-Israa 17:85

الإسراء

وَيَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلرُّوحِ ۖ قُلِ ٱلرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّى وَمَآ أُوتِيتُم مِّنَ ٱلْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا

Maana

Na wanakuuliza habari za Roho. Sema, "Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika elimu isipokuwa kidogo tu."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo tu. [85]

[85] Ewe Muhammad! Watu wako wanakuuliza kwa kutomezwa na Mayahudi: Nini hakika ya Roho? Waambie: Roho ni katika ilimu yake Mwenyewe Mola wangu Mlezi aliyo jikhusisha nayo Yeye. Na nyinyi hamkupewa ilimu ila chache tu ukilinganisha na ilimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na makafiri wanakuuliza juu ya uhakika wa roho kwa njia ya ushindani, basi wajibu kwamba uhakika wa roho na hali zake ni katika mambo ambayo Allah Mtukufu Ameufanya ujuzi wake uweko Kwake. Na hamkupewa ujuzi, nyinyi na watu wote, isipokuwa kitu kichache.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net