Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 86

Al-Israa 17:86

الإسراء

وَلَئِن شِئْنَا لَنَذْهَبَنَّ بِٱلَّذِىٓ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ بِهِۦ عَلَيْنَا وَكِيلًا

Maana

Na tungelipenda, tungeliyaondoa yale tuliyokufunulia. Kisha usingelipata mwakilishi wa kukupigania kwetu kwa haya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tungeli penda tungeli yaondoa tuliyo kufunulia. Kisha usingeli pata mwakilishi wa kukupigania kwetu kwa haya. [86]

[86] Na lau tungeli taka kuifuta kabisa kifuani mwako hiyo Qur'ani tuliyo kufunulia tungeli fanya hivyo, na kisha usingeli mpata yeyote wa kukunusuru katika watu wako.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau tungetaka kuifuta Qur’ani moyoni mwako, tungaliliweza hilo, na hungalimpata mwenye kukuhami ambaye angetuzuia kufanya hivyo au akurudishie Qur’ani.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net