Al-Israa 17:87
الإسراءإِلَّا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ إِنَّ فَضْلَهُۥ كَانَ عَلَيْكَ كَبِيرًا
Isipokuwa iwe rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika fadhila yake kwako ni kubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Isipo kuwa iwe rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika fadhila yake kwako ni kubwa. [87]
[87] Lakini tumeiacha Qur'ani ibaki vile vile kifuani mwako kwa rehema kutoka kwa Mola wako Mlezi, kwani fadhila zake kwako wewe ni kubwa mno katika muujiza huu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Lakini Allah Mtukufu Alikurehemu, Akaithibitisha moyoni mwako, hakika wema Wake juu yako ni mkubwa. Yeye Amekupa hii Qur’ani tukufu, Al-Maqãm al-Maḥmûd (Kisimamo Kishukuriwacho) na mengineyo miongoni mwa yale ambayo Hakumpa yoyote katika viumbe.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net