Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Israa
Sura ya 17

Al-Israa

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 83

وَإِذَآ أَنْعَمْنَا عَلَى ٱلْإِنسَـٰنِ أَعْرَضَ وَنَـَٔا بِجَانِبِهِۦ ۖ وَإِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ كَانَ يَـُٔوسًا 83

{83} Haya ndiyo maumbile ya asili ya mtu kama alivyo, isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu alimuongoa. Kwa maana mtu anaponeemeshwa na Mwenyezi Mungu, hufurahia neema hizo, na huzifanyia kiburi na hukengeuka na kujiweka mbali na Mola wake Mlezi. Hamshukuru, wala hamtaji. "Na yanapomgusa maovu" kama vile maradhi na mengineyo, "Hukata tamaa" ya kupata heri, na akawa amekata matumaini yake kwa Mola wake Mlezi, na akadhani kwamba yale aliyomo yatadumu milele. Na ama yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, yeye wakati anaponeemeshwa, humnyenyekea Mola wake Mlezi na anamshukuru kwa neema zake. Na wakati wa shida, huomba dua kwa unyenyekevu, na kutaraji salama kutoka kwa Mwenyezi Mungu kumuondolea yale yanayompata, na kwa hayo dhiki hiyo inakuwa nyepesi kwake.