Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 82

Al-Israa 17:82

الإسراء

وَنُنَزِّلُ مِنَ ٱلْقُرْءَانِ مَا هُوَ شِفَآءٌ وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ۙ وَلَا يَزِيدُ ٱلظَّـٰلِمِينَ إِلَّا خَسَارًا

Maana

Na tunateremsha katika Qur-ani yale ambayo ni uponyaji na rehema kwa Waumini. Wala hayawazidishii madhalimu isipokuwa hasara.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tunateremsha katika Qur'ani yaliyo ni matibabu na rehema kwa Waumini. Wala hayawazidishii madhaalimu ila khasara. [82]

[82] Na vipi Haki isiwe na nguvu na hali Sisi tunateremsha katika Qur'ani dawa ya kuponyesha maradhi ya shaka katika vifua vya watu, na sababu za kuwapatia rehema wanao iamini! Na madhaalimu hawana linao wazidia ila khasara tu kwa kuikataa kwao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tunateremsha miongoni mwa aya za Qur’ani yanayopoza magonjwa ya nyoyo kama shaka, unafiki na ujinga, na yanayopoza miili kwa kujitibu nayo, na yanayokuza Imani ambayo ni sababu ya kufaulu kupata rehema za Allah Mtukufu. Na hii Qur’ani haiwaongezei makafiri wanapoisikia isipokua ukafiri na upotevu, kwa kuikanusha kwao na kutoiamini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net