Al-Israa 17:81
الإسراءوَقُلْ جَآءَ ٱلْحَقُّ وَزَهَقَ ٱلْبَـٰطِلُ ۚ إِنَّ ٱلْبَـٰطِلَ كَانَ زَهُوقًا
Na sema, "Haki imefika, na batili imetoweka. Hakika batili lazima itoweke!"
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke! [81]
[81] Na sema ukiwaonya watu wako washirikina: Haki ya Tawhid, Imani ya Mungu Mmoja, na Dini ya Kweli na Uadilifu, imekwisha fika. Na uwongo, na ushirikina, na dini ya ufisadi na dhulma, yote hayo yameondoka. Kwani uwongo daima hauna dawamu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na useme, ewe Mtume, kuwaambia washirikina, «Uislamu umekuja na ushirikina umeondoka. Kwani ubatilifu hauna kusalia wala kujikita, na ukweli ndio wenye kuimarika na kusalia ambao hauondoki».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net