Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 80

Al-Israa 17:80

الإسراء

وَقُل رَّبِّ أَدْخِلْنِى مُدْخَلَ صِدْقٍ وَأَخْرِجْنِى مُخْرَجَ صِدْقٍ وَٱجْعَل لِّى مِن لَّدُنكَ سُلْطَـٰنًا نَّصِيرًا

Maana

Na sema, "Mola wangu Mlezi! Niingize muingizo mwema, na unitoe kutoka kwema. Na unipe nguvu zinazotoka kwako zinisaidie."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na sema: Mola wangu Mlezi! Niingize muingizo mwema, na unitoe kutoka kwema. Na unipe nguvu zinazo toka kwako zinisaidie. [80]

[80] Na sema: Ewe Mola Mlezi! Niingize maingizo ya kuridhisha matukufu katika kila unapo niingiza katika jambo au pahala. Na unitoe kwa kutoka kunako ridhisha kutukufu. Na kwa fadhila yako nijaalie nguvu za kunisaidia niwashinde maadui zangu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na useme, «Mola wangu! niingize maingizo mazuri katika jambo lililo jema kwangu na unitoe matoko mazuri kwenye mambo yaliyo mabaya kwangu, na unipatie hoja thabiti kutoka kwako yenye kuniokoa na wote wanaoenda kinyume na mimi». Na hivyo ndivyo ilivyokuwa, kwani haukupita mu (rehma za Allah Mtukufu na amani zimshukie) k Akawakusanya na wao hapo Badr, hapo wakubw Tazama Ibn Kathîr katika kufasiri aya hii.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net