Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 79

Al-Israa 17:79

الإسراء

وَمِنَ ٱلَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِۦ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰٓ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا

Maana

Na amka usiku kwa ajili ya kufanya ibada kwayo, ni ziada ya sunna hasa kwako wewe. Huenda Mola wako Mlezi akakunyanyua cheo kinachosifika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na amka usiku kwa ibada; ni ziada ya sunna khasa kwako wewe. Huenda Mola wako Mlezi akakunyanyua cheo kinacho sifika. [79]

[79] Na katika wakati wa usiku amka, kwa kusali Swala ya Tahajjud. Hiyo ni ibada ya zaidi juu ya zile Swala Tano. Hii imekukhusu wewe tu, kwa kutaraji kuwa Mola wako Mlezi atakuweka Siku ya Kiyama makamo watakao kusifia viumbe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na inuka, ewe Nabii, kutoka kwenye usingizi sehemu ya usiku, usome Qur’ani katika Swala ya usiku, ipate kuwa, hiyo Swala ya usiku, ni nyongeza kwako katika utukufu wa cheo na kupandishwa daraja. Huenda Allah Mtukufu Akakuleta uwe ni mwenye kuwaombea msamaha watu Siku ya Kiyama, ili Allah Mtukufu Awarehemu kwa kuwaondolea waliokuwa nayo, na usimame kisimamo ambacho watakushukuru kwacho wa mwanzo na wa mwisho.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net