Al-Israa 17:78
الإسراءأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ لِدُلُوكِ ٱلشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ ٱلَّيْلِ وَقُرْءَانَ ٱلْفَجْرِ ۖ إِنَّ قُرْءَانَ ٱلْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا
Simamisha Swala jua linapopinduka mpaka giza la usiku, na Qur-ani ya alfajiri. Hakika Qur-ani ya alfajiri inashuhudiwa daima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Shika Swala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur'ani ya al fajiri. Hakika Qur'ani ya alfajiri inashuhudiwa daima. [78]
[78] Shika Swala zilizo faridhiwa, tangu kupinduka jua kati ya mbingu kuelekea upande wa machwea jua, mpaka kiza cha usiku. Na hizi ndizo Swala za Adhuhuri, Alasiri, Magharibi na Isha. Na pia shika Swala ya Alfajiri ambayo wanaishuhudia Malaika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Simamisha Swala itimie kuanzia kipindi cha kupinduka jua wakati wa mchana mpaka kipindi cha usiku. Inaingia hapa Swala ya Adhuhuri, Alasiri, Magharibi na Isha. Na simamisha Swala ya Alfajiri na urefushe kisomo chake, kwani Swala ya Alfajiri inahudhuriwa na Malaika wa usiku na Malaika wa mchana.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net