Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 77

Al-Israa 17:77

الإسراء

سُنَّةَ مَن قَدْ أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِن رُّسُلِنَا ۖ وَلَا تَجِدُ لِسُنَّتِنَا تَحْوِيلًا

Maana

Hiyo ndiyo desturi ya Mitume wetu tuliowatuma kabla yako. Wala hutapata mabadiliko katika desturi yetu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Huo ndio mwendo kwa Mitume tulio watuma kabla yako. Wala hupati mabadiliko katika mwendo wetu [77]

[77] Na huo ndio mwendo wetu kwa Mitume wa kabla yako - huwahiliki wale wanao wafukuza Manabii wao. Na wala hapana mabadiliko katika mwendo wetu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Huo ndio mwendo uliowekwa na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, katika kuwaangamiza watu wanaomtoa Mtume wao kutoka kwao, na hutapata mabadiliko kwenye mwendo wetu, kwani hatuendi kinyume na ahadi yetu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net