Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 76

Al-Israa 17:76

الإسراء

وَإِن كَادُوا۟ لَيَسْتَفِزُّونَكَ مِنَ ٱلْأَرْضِ لِيُخْرِجُوكَ مِنْهَا ۖ وَإِذًا لَّا يَلْبَثُونَ خِلَـٰفَكَ إِلَّا قَلِيلًا

Maana

Na walitaka kukukera ili wakutoe nchini. Na hapo, wao wasingelibakia humo isipokuwa kwa muda mchache tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walitaka kukukera ili uitoke nchi. Na hapo wao wasingeli bakia humo ila kwa muda mchache tu. [76]

[76] Na makafiri wa Makka wamejaribu, na walikaribia kukuudhi mpaka wakutoe kwenye ardhi ya Makka kwa uadui wao na chuki zao. Na lau yangeli kuwa hayo, basi wao nao wasingeli baki humo ila muda mchache tu, kisha washindwe katika hayo mambo yao, na hukumu iwe ya Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na makafiri walikaribia kukutoa Makkah kwa kukukera, na lau wangekutoa huko hawangalikaa huko baada yako isipokuwa muda mchache, hadi iwashukie adhabu ya ulimwenguni.(1) 1 Tafsiri ya aya hii yategemea moja ya sababu zil kuwa makafiri wa kikureshi walitaka kumtoa Mtum zimshukie) kwenye mji, Allah Mtukufu Akawao wangemtoa hawangalikaa kwenye mji wa Makkah

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net