Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 75

Al-Israa 17:75

الإسراء

إِذًا لَّأَذَقْنَـٰكَ ضِعْفَ ٱلْحَيَوٰةِ وَضِعْفَ ٱلْمَمَاتِ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ عَلَيْنَا نَصِيرًا

Maana

Hapo basi bila ya shaka, tungelikuonjesha adhabu maradufu ya uhai, na adhabu maradufu ya kifo. Kisha usingepata yeyote wa kukunusuru kutokana nasi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hapo basi bila ya shaka tungeli kuonjesha adhabu mardufu ya uhai, na adhabu mardufu ya kifo. Kisha usinge pata mtu wa kukunusuru nasi. [75]

[75] Na lau ungeli karibia kuwaelekea hao, basi tungeli kukusanyia adhabu za duniani tukazifanya mardufu, na adhabu za Akhera nazo tukaziongeza mara mbili vile vile. Na wala usingeli pata yeyote wa kukunusuru na adhabu. Lakini hayo hayawi kabisa, hayawezi kumfikilia Mtume wetu Muaminifu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau ungeelemea, ewe Mtume, upande wa hawa washirikina maelemeo madogo katika yale waliyotaka kwako, basi tungalikuonjesha mara mbili zaidi ya adhabu ya duniani na mara mbili zaidi ya adhabu ya baada ya kufa kesho Akhera, hivyo ni kwa ajili ya kutimia neema ya Allah Mtukufu kwako na ukamilifu wa kumjua Mola wako, kisha hutampata yoyote mwenye kukuepushia adhabu yetu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net