Al-Israa 17:74
الإسراءوَلَوْلَآ أَن ثَبَّتْنَـٰكَ لَقَدْ كِدتَّ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْـًٔا قَلِيلًا
Na lau kuwa hatukukuweka imara, ungelikaribia kuwaegemea kidogo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na lau kuwa hatukukuweka imara ungeli karibia kuwaelekea kidogo. [74]
[74] Upole wetu umekugubika wewe, tukakulinda usiwakubalie matakwa yao, na tukakupa nguvu usimame juu ya Haki. Na lau kuwa si hayo ungeli karibia kuwakubalia kwa tamaa ya kuwa huenda ikafika siku imani yao ikakamilika baadae wakisha anza kuingia katika Uislamu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau si sisi kukuimarisha kwenye haki na kukuhifadhi usikubaliane nao, ungalikaribia kuelemea kwao kidogo katika yale waliyokushauri kwa nguvu za udanganyifu wao na wingi wa hila zao na kuwa na hamu kwako waongoke.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net