Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 73

Al-Israa 17:73

الإسراء

وَإِن كَادُوا۟ لَيَفْتِنُونَكَ عَنِ ٱلَّذِىٓ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ لِتَفْتَرِىَ عَلَيْنَا غَيْرَهُۥ ۖ وَإِذًا لَّٱتَّخَذُوكَ خَلِيلًا

Maana

Na hakika walikaribia kukushawishi uache hayo tuliyokufunulia ili utuzulie mengineyo. Na hapo, ndipo wangelikufanya mwandani.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika walikaribia kukushawishi uache tuliyo kufunulia ili utuzulie mengineyo. Na hapo ndio wangeli kufanya rafiki. [73]

[73] Hakika washirikina wanatafuta kila njia wakuachishe Qur'ani utafute miujiza myengineyo, ili uwe kama uliye tuzulia Sisi uwongo. Na hapo ndio watakufanya uwe rafiki yao! Na hila hizi zimekaririwa na zimekuwa nyingi. Na kwa hivyo ungeli karibia kuyafuata wayatakayo, ila kwa kuwa wewe ni Mtume wetu uliye muaminifu, hayakuwa hayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa hakika washirikina walikaribia kukuepusha, ewe Mtume, na Qur’ani Aliyokuteremshia Allah Mtukufu ili utuzulie isiyokuwa hiyo tuliyokuletea wahyi nayo. Na lau ungefanya walivyotaka, wangalikufanya ni kipenzi mwenye kusifiwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net