Al-Israa 17:72
الإسراءوَمَن كَانَ فِى هَـٰذِهِۦٓ أَعْمَىٰ فَهُوَ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ أَعْمَىٰ وَأَضَلُّ سَبِيلًا
Na yule ambaye ni kipofu hapa, basi atakuwa kipofu Akhera, na atakuwa ndiye mpotovu zaidi wa Njia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na aliye kuwa hapa kipofu, basi atakuwa kipofu Akhera, na atakuwa aliye ipotea zaidi Njia. [72]
[72] Ama yule wa kikundi kingine yatamhuzunisha atayo yaona. Na atazibiwa njia za kuokoka. Na atakuwa kipofu asione pa kuepuka adhabu yake, kama alivyo kuwa duniani kipofu haioni Njia ya Haki na Uwongofu! Na anaye kuwa duniani kipofu (wa moyo) basi Akhera ni kipofu zaidi, na yu mbali zaidi na Njia ya Kheri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na aliyekuwa kipofu wa moyo, katika ulimwengu huu, wa kutoziona dalili za uwezo wa Allah Mtukufu, asiyaamini yale aliyokuja nayo Mtume Muhammad, (rehema na amani zimshukie), basi yeye, Siku ya Kiyama, atakuwa kipofu zaidi wa kutoiona njia ya Peponi na atapotea zaidi njia ya uongofu na usawa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net