Al-Israa 17:71
الإسراءيَوْمَ نَدْعُوا۟ كُلَّ أُنَاسٍۭ بِإِمَـٰمِهِمْ ۖ فَمَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ يَقْرَءُونَ كِتَـٰبَهُمْ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا
Siku tutakapoita kila kikundi cha watu kwa mujibu wa wakifuatacho, basi atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, basi hao watasoma kitabu chao wala hawatadhulumiwa hata chembe.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Siku tutapo waita kila kikundi cha watu kwa mujibu wa wakifuatacho - basi atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, basi hao watasoma kitabu chao wala hawatadhulumiwa hata chembe. [71]
[71] Ewe Nabii! Waambie watu wako: Siku tutapo waita kila kikundi kwa alama zao wanazo zijua, au mwongozi wao wanaye mfuata, au Nabii, au Kitabu wakaambiwa: Enyi watu wa Musa! Au Enyi watu wa Qur'ani! Na kadhaalika, ili wapokee vitabu vya a'mali zao. Basi atakaye pokea kitabu cha a'mali zake kwa mkono wake wa kulia, na hao ndio wenye bahati njema, hao watasoma kitabu chao kwa furaha. Na wala hawatapunguziwa katika ujira wao duni ya kitu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka, ewe Mtume, Siku ya Kufufuliwa, kwa njia ya kutoa bishara na kuogopesha, pindi Allah Mtukufu, Aliyeshinda na kutukuka, Atakapoliita kila kundi la watu pamoja na kiongozi wao ambaye walikuwa wakimfuata ulimwenguni. Basi aliyekuwa mwema kati yao, na akapewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, hawa watasoma kitabu cha mema yao wakiwa katika hali ya kufurahika na kuwa na bishara njema, na kamwe hawatapunguziwa chochote katika malipo ya matendo yao mazuri, hata kama ni kadiri ya uzi unaokuwa kwenye mpasuko wa koko ya tende.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net