Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 70

Al-Israa 17:70

الإسراء

وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِىٓ ءَادَمَ وَحَمَلْنَـٰهُمْ فِى ٱلْبَرِّ وَٱلْبَحْرِ وَرَزَقْنَـٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَـٰتِ وَفَضَّلْنَـٰهُمْ عَلَىٰ كَثِيرٍ مِّمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلًا

Maana

Na hakika tumewatukuza wanadamu, na tukawabeba katika nchi kavu na baharini, na tukawaruzuku katika vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa wale tuliowaumba.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba. [70]

[70] Na hakika Sisi tumewatukuza wana wa Adam kwa kuwapa umbo zuri lilio nyooka, na matamshi, na uwezo wa kukhiari mambo. Na tukawapa hishima na utukufu pindi wakit'ii. Na tukawapakia nchi kavu juu ya wanyama, na baharini katika marikebu, na tukawaruzuku vitu vitamu, na tukawafadhilisha fadhila kubwa kuliko viumbe vingi kwa kuwapa akili na kuweza kufikiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika tumewatukuza watu wa kizazi cha Ãdam kwa akili na kuwapelekea Mitume, na tukawadhalilishia vilivyoko ulimwenguni vyote: tukawadhalilishia wanyama barani wa kuwapanda na vyombo baharini vya kuwabeba, tukawaruzuku vilaji na vinywaji vizuri na tukawapa daraja kubwa juu ya viumbe wengi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net