Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 8

Al-Israa 17:8

الإسراء

عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يَرْحَمَكُمْ ۚ وَإِنْ عُدتُّمْ عُدْنَا ۘ وَجَعَلْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَـٰفِرِينَ حَصِيرًا

Maana

Huenda Mola wenu Mlezi akakurehemuni, na mkirudia, na sisi tutarudia. Na tumeifanya Jahannam kuwa ni gereza kwa ajili ya makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Huenda Mola wenu Mlezi akakurehemuni. Na mkirudia na Sisi tutarudia. Na tumeifanya Jahannamu kuwa ni gereza kwa ajili ya makafiri. [8]

[8] Asaa Mola wenu Mlezi akakurehemuni baada ya hiyo mara ya pili pindi mkitubu. Na mkirejea kwenye ufisadi Nasi tutarejea kukuadhibuni. Na tumeifanya Jahannam kuwa ndiyo gereza la kuwafungia makafiri!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Inatarajiwa kuwa Mola wenu, enyi Wana wa Isrãîl, Atawarehemu baada ya kuwatesa, mkitubia na mkatengenea, na mkirudi kufanya uharibifu na maonevu, tutarudi kuwatesa na kuwadhili. Na tumeufanya moto wa Jahanamu, kwenu na kwa makafiri kwa jumla, ni gereza ambalo hakuna kutoka humo kabisa. Katika aya hii na ile kabla yake pana onyo kwa ummah huu dhidi ya kufanya maasia ili lisiwapate lile lililowapata Wana wa Isrãîl, basi mipango ya Allah Mtukufu ni mimoja, haina kubadilika wala kugeuka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net