Al-Israa 17:9
الإسراءإِنَّ هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانَ يَهْدِى لِلَّتِى هِىَ أَقْوَمُ وَيُبَشِّرُ ٱلْمُؤْمِنِينَ ٱلَّذِينَ يَعْمَلُونَ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا كَبِيرًا
Hakika hii Qur-ani inaongoa kwenye yale yaliyonyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba wana malipo makubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye ya yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa. [9]
[9] Hakika hii Qur'ani inawaongoza watu kwenye njia ambayo ndiyo njia iliyo kaa sawa kabisa kuliko njia zote, na ndiyo njia ya salama kabisa ya kufikilia kwenye furaha ya kweli katika dunia. Na wabashirie wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wenye kuit'ii Haki na wanatenda vitendo vyema, kuwa watapata ujira mkubwa Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika hii Qur’ani tuliyoiteremsha kwa mja wetu Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), inawaongoza watu kwenye njia nzuri kabisa nayo ni mila ya Kiislamu, na inawapa bishara njema Waumini, wanaofanya yale ambayo Allah Mtukufu Amewaamrisha kwayo na wanaokomeka na yale ambayo Amewakataza nayo, kwamba watakuwa na malipo makubwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net