Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 7

Al-Israa 17:7

الإسراء

إِنْ أَحْسَنتُمْ أَحْسَنتُمْ لِأَنفُسِكُمْ ۖ وَإِنْ أَسَأْتُمْ فَلَهَا ۚ فَإِذَا جَآءَ وَعْدُ ٱلْـَٔاخِرَةِ لِيَسُـۥٓـُٔوا۟ وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا۟ ٱلْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا۟ مَا عَلَوْا۟ تَتْبِيرًا

Maana

Mkifanya wema, mnafanyia wema nafsi zenu. Na mkifanya ubaya, basi mnajifanyia wenyewe. Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu na waingie Msikitini kama walivyoingia mara ya kwanza na waharibu kila walichokiteka kwa uharibifu mkubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi mkifanya wema, mnajifanyia wema nafsi zenu. Na mkifanya ubaya, mnajifanyia wenyewe. Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa. [7]

[7] Na tukawambia: Mkifanya wema na mkamt'ii Mwenyezi Mungu, wema wenu utakufaeni nafsi zenu duniani na Akhera. Na mkifanya uovu kwa maasi, basi mnajiharibia nafsi zenu vile vile. Na utapo kuja wakati wa adhabu pale mara ya mwisho katika zile mara mbili za ufisadi wenu katika nchi, tutakupelekeeni maadui zenu, wafanye athari za uovu na madhila na huzuni zidhihiri nyusoni mwenu. Na matokeo yake ni kuingia katika Msikiti wa Baitul Muqaddas, wakauharibu kama walivyo ingia na wakauharibu mara ya kwanza, wakateketeza watacho kipata kwa uteketezi mkubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mkifanya matendo yenu na maneno yenu kuwa mazuri,basi mmejifanyia vizuri nyinyi wenyewe, kwa kuwa malipo ya hayo yatarudi kwenu; na mkifanya vibaya, basi mateso ya hayo ni yenye kuwarudia nyinyi. Na utakapofika wakati wa uharibifu wa pili, tutawasaliti maadui wenu mara nyingine, ili wawadhalilishe na wawashinde na idhihiri athari ya udhalilifu na utwevu kwenye nyuso zenu na wawaingilie kwenye Bayt al Maqdis waiharibu kama walivyoiharibu mara ya kwanza na wavunjevunje kila kilichoko chini ya mikono yao uvunjaji kamili.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net