Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 6

Al-Israa 17:6

الإسراء

ثُمَّ رَدَدْنَا لَكُمُ ٱلْكَرَّةَ عَلَيْهِمْ وَأَمْدَدْنَـٰكُم بِأَمْوَٰلٍ وَبَنِينَ وَجَعَلْنَـٰكُمْ أَكْثَرَ نَفِيرًا

Maana

Kisha tukawarudishia nguvu zenu dhidi yao, na tukawasaidia kwa mali na wana, na tukawafanya kuwa wengi zaidi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukakurudishieni nguvu zenu dhidi yao, na tukakusaidieni kwa mali na wana, na tukakujaalieni mkawa wengi zaidi. [6]

[6] Kisha mambo yenu yalipo kaa sawa, na mkaongoka, na mkatengeneza umoja wenu, na mkaacha ufisadi, tukakurejezeeni ushindi juu ya wale makhasimu zenu. Nasi tukakuruzukuni mali na wana, na mkazidi kuwa wingi kwa idadi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukawarudishia ushindi, enyi wana wa Isrãîl, na kuwa juu ya maadui zenu waliowasaliti, na tukawazidishia riziki zenu na watoto wenu na tukawapa nguvu na tukawafanya muwe wengi wa idadi kuliko adui yenu. Hiyo ni kwa sababu ya wema wenu na unyenyekevu wenu kwa Mola wenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net