Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 5

Al-Israa 17:5

الإسراء

فَإِذَا جَآءَ وَعْدُ أُولَىٰهُمَا بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ عِبَادًا لَّنَآ أُو۟لِى بَأْسٍ شَدِيدٍ فَجَاسُوا۟ خِلَـٰلَ ٱلدِّيَارِ ۚ وَكَانَ وَعْدًا مَّفْعُولًا

Maana

Na itakapokuja ahadi ya kwanza yake, tutawatumia waja wetu wenye nguvu kubwa. Watawaingilia ndani ya majumba. Na hii ilikuwa ahadi iliyotimizwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi itapo fika ahadi ya kwanza yake tutakupelekeeni waja wetu wa kali kwa vita. Watakuingilieni ndani ya majumba. Na hii ilikuwa ahadi iliyo timizwa. [5]

[5] Na ulipo fika wakati wa kukuleteeni adhabu mara ya kwanza, tulikupatilizeni, kwa sababu ya fisadi yenu, kwa kukusalitishieni watu wa kali kupigana. Wakakuingilieni mpaka ndani ya majumba, hapana walicho kiacha, ili wakuuweni. Na ahadi ya kukuadhibuni ilikuwa ni ahadi haina budi kutimizwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ukitokea kutoka kwenu uharibifu wa kwanza, tutawasaliti nyinyi na waja wetu wenye ushujaa na nguvu kali, watawashinda, watawaua na watawafukuza, hapo wazunguke kwenye nyumba zenu wakifanya uharibifu. Hiyo ilikuwa ni ahadi isiyokuwa na budi kutokea kwa kupatikana sababu zake kutoka kwenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net