Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 4

Al-Israa 17:4

الإسراء

وَقَضَيْنَآ إِلَىٰ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ فِى ٱلْكِتَـٰبِ لَتُفْسِدُنَّ فِى ٱلْأَرْضِ مَرَّتَيْنِ وَلَتَعْلُنَّ عُلُوًّا كَبِيرًا

Maana

Na tukawahukumia Wana wa Israili katika Kitabu kwamba hakika mtafanya uharibifu katika ardhi mara mbili, na hakika mtapanda kiburi, kupanda kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukawahukumia Wana wa Israili katika Kitabu kwamba: Hakika nyinyi mtafanya fisadi katika nchi mara mbili, na kwa yakini mtapanda kiburi, kiburi kikubwa. [4]

[4] Na tukatekeleza hukumu yetu kwa Wana wa Israili katika tuliyo yaandika katika Lauhun Mahfuudh, Ubao Ulio Hifadhiwa, ya kwamba watafanya ufisadi katika Nyumba Takatifu (Baitul Muqaddas) bila ya shaka yoyote mara mbili. Kila mara katika hizo itakuwa ni udhaalimu na uasi, na kuacha hukumu za Taurati, na kuwauwa Manabii, na mtasaidiana katika madhambi, na kwamba utawala wenu utaenea, na kutukuka na kupanda kichwa na kiburi kwa dhulma zenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tuliwapasha habari Wana wa Isrãîl katika Taurati ambayo waliteremshiwa kwamba hapana budi utatokea kutoka kwao uharibifu mara mbili katika Bayt al-Maqdis na sehemu zinazofuatia kwa kudhulumu, kuua Manabii, kufanya kiburi, kupita kiasi na kufanya uadui.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net