Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Israa
Sura ya 17

Al-Israa

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 4

وَقَضَيْنَآ إِلَىٰ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ فِى ٱلْكِتَـٰبِ لَتُفْسِدُنَّ فِى ٱلْأَرْضِ مَرَّتَيْنِ وَلَتَعْلُنَّ عُلُوًّا كَبِيرًا 4

{4} "Na tukawahukumia Wana wa Israili." Yaani, tulichukua ahadi yao na tukawaambia katika kitabu chao kwamba lazima utatokea uharibifu miongoni mwa katika ardhi mara mbili kwa kufanya maasia, na kujivuna kwa sababu ya neema za Mwenyezi Mungu na kupanda kiburi katika ardhi na kutakabari humo, na kwamba moja tu ya hayo itakapofanyika, basi Mwenyezi Mungu atawapa mamlaka maadui zao dhidi yao na kuwaadhibu. Na hili ni tahadharisho kwao na onyo ili labda watarudi na kukumbuka.