Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 3

Al-Israa 17:3

الإسراء

ذُرِّيَّةَ مَنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَبْدًا شَكُورًا

Maana

Kizazi cha wale tuliowabeba pamoja na Nuhu. Hakika yeye alikuwa mja wa kushukuru sana.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi kizazi tuliyo wachukua pamoja na Nuhu! Hakika yeye alikuwa mja mwenye shukrani. [3]

[3] Nyinyi Wana wa Israili mmezalikana kutokana na wale watu safi wema walio kuwa na Nuhu katika safina baada ya kuwa wameamini. Nasi tukawaokoa wasizame. Basi mfanyeni Nuhu kuwa ndiye mwongozi wenu wa kumfuata, kama walivyo mfanya wazee wenu walio tangulia. Kwani hakika yeye alikuwa mja wa wingi wa shukrani kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi kizazi cha wale tuliowaokoa na tukawabeba pamoja na Nûḥ katika jahazi, msimshirikishe Allah Mtukufu katika kumuabudu, na kuweni ni wenye kushukuru neema Zake na ni wenye kumfuata Nûḥ, amani imshukie, kwani yeye alikuwa ni mja mwenye kumshukuru Allah Mtukufu kwa moyo wake, ulimi wake na viungo vyake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net