Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 2

Al-Israa 17:2

الإسراء

وَءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ وَجَعَلْنَـٰهُ هُدًى لِّبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ أَلَّا تَتَّخِذُوا۟ مِن دُونِى وَكِيلًا

Maana

Na tulimpa Musa Kitabu na tukakifanya kuwa ni uongofu kwa Wana wa Israili. (Tukawaambia) kwamba msimfanye yeyote asiyekuwa mimi kuwa mtegemewa wenu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukampa Musa Kitabu, na tukakifanya uwongofu kwa Wana wa Israili. (Tukawambia): Msiwe na mtegemewa ila Mimi! [2]

[2] Na hakika hiyo Baitul Muqaddas ilikuwa inakaliwa na Wana wa Israili baada ya Musa, mpaka walipo fanya fisadi yao humo, wakafukuzwa hapo zamani. Haya ijapo kuwa Sisi tulimpa Musa Taurati, na tukatia ndani yake uwongofu, na tukawaambia: Msimfanye yeyote wa kumtegemezea mambo yenu isipo kuwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kama Allah Mtukufu Alivyomtukuza Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa kumpeleka safari hiyo ya usiku, Alimtukuza Mûsã, amani imshukie, kwa kumpa Taurati na Akaifanya ni yenye kuufafanua ukweli na kuwaongoza Wana wa Isrãîl na Akaifanya ni yenye kukusanya makatazo kwao ya kumfanya asiyekuwa Allah Mtukufu kuwa ni mtegemewa au ni muabudiwa wakawa wamtegemezea mambo yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net