Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 1

Al-Israa 17:1

الإسراء

سُبْحَـٰنَ ٱلَّذِىٓ أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِۦ لَيْلًا مِّنَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ إِلَى ٱلْمَسْجِدِ ٱلْأَقْصَا ٱلَّذِى بَـٰرَكْنَا حَوْلَهُۥ لِنُرِيَهُۥ مِنْ ءَايَـٰتِنَآ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْبَصِيرُ

Maana

Ametakasika yule aliyemsafirisha mja wake usiku mmoja kutoka katika Msikiti Mtakatifu mpaka Msikiti wa Al-Aqswa, ambao tumebariki kandoni mwake, ili tumuonyeshe katika Ishara zetu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia zaidi, Mwenye kuona mno.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona. [1]

[1] Mwenyezi Mungu aliye takasika na kila ambalo lisio laiki naye. Yeye ndiye aliye mchukua mja wake Muhammad wakati wa usiku kutoka Msikiti Mtakatifu wa Makka kwendea Msikiti wa Mbali wa Baitul Muqaddas, ambao tuliwabarikia wakaazi majirani wa Msikiti huo katika mahitaji yao, ili tumwonyeshe baadhi ya Ishara zetu zenye ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kuwa Mimi ni Mungu Mmoja peke yangu, na ukubwa wa uwezo wangu! Hakika Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kuona.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Anajisifu na kujitukuza kwa uwezo Wake juu ya yasiyowezekana na yoyote isipokuwa Yeye, hapana Mola isipokuwa Yeye, hapana Mlezi isipokuwa Yeye. Yeye Ndiye ambaye alimpeleka mja Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kipindi cha usiku, kwa mwili wake na roho yake, katika hali ya kuwa macho na siyo ya kulala, kutoka msikiti wa Ḥarãm Uliyoko Makkah, kwenda msikiti wa Aqṣã uliyoko Bayt al- Maqdis, ambao Allah Mtukufu Amezibariki sehemu zinazouzunguka kwa matunda, nafaka na vinginevyo, na Akaufanya ni mahali pa Manabii wengi, ili ajionee maajabu ya uwezo wa Allah Mtukufu na dalili za upweke Wake. Hakika Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, Ndiye Mwenye kuzisikia sauti zote, Ndiye Mwenye kukiona kila cha kuonekana, na Atampa kila mmoja anachofaa kupata duniani na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net