An-Nahl 16:128
النحلإِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوا۟ وَّٱلَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ
Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na wale watendao mazuri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na watendao mema. . [128]
[128] Kwani hakika Mola wako Mlezi yu pamoja na wale wanao jikinga na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kuyaepuka anayo yakataza, na wakazifanya a'mali zao ziwe nzuri kwa sababu ya Mwenyezi Mungu kwa kukubali kumt'ii. Yeye atawanusuru duniani, na Akhera atawalipa bora ya malipo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, kwa taufiki Yake, msaada Wake, upaji nguvu Wake na nusura Yake Yuko pamoja na waliomcha kwa kuyafuata Aliyoyaamrisha na kuyaacha Aliyoyakataza; na yuko pamoja na wale wanaotenda wema, kwa kutekeleza faradhi Zake na kusimama kutimiza haki Zake na kujilazimisha kumtii, kwa kuwapa msaada Wake, uongofu Wake na nusura Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net