Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 91

An-Nahl 16:91

النحل

وَأَوْفُوا۟ بِعَهْدِ ٱللَّهِ إِذَا عَـٰهَدتُّمْ وَلَا تَنقُضُوا۟ ٱلْأَيْمَـٰنَ بَعْدَ تَوْكِيدِهَا وَقَدْ جَعَلْتُمُ ٱللَّهَ عَلَيْكُمْ كَفِيلًا ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ

Maana

Na timizeni agano la Mwenyezi Mungu mnapoagana, wala msivunje viapo baada ya kuvifunga imara, ilhali mmekwishamfanya Mwenyezi Mungu ndiye mdhamini wenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua myafanyayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na timizeni ahadi ya Mwenyezi Mungu mnapo ahidi, wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha, ilihali mmekwisha mfanya Mwenyezi Mungu ndiye mdhamini wenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua myatendayo. [91]

[91] Na timizeni ahadi mlizo jitolea nafsi zenu kwa kumshuhudisha Mwenyezi kuwa mtazitekeleza, maadamu ahadi hizo ni kwa mujibu wa sharia ya Mwenyezi Mungu. Wala msivunje viapo vyenu kwa kutotimiza baada ya kuvitilia nguvu kwa kumtaja Mwenyezi Mungu, na kuazimia kikweli kutimiza. Nanyi mlipo toa ahadi mlitia maanani kuwa Mwenyezi Mungu ndiye dhamini wenu kwamba mtatekeleza, na kwamba Mwenyezi Mungu anakuangalieni na kukuoneni. Basi shikamaneni na ahadi zenu na viapo vyenu, kwani Mwenyezi Mungu Subhanahu anakujueni yupi katika nyinyi anaye timiza na anaye kwenda kinyume, yupi anaye tekeleza na yupi anaye vunja. Basi atakulipeni kwa mnayo yafanya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na jilazimisheni kutekeleza kila ahadi mliyojilazimisha nayo juu ya nafsi zenu, baina yenu nyinyi na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, au baina yenu na watu katika yale yasiyoenda kinyume na Kitabu cha Allah Mtukufu na Sunnah ya Nabii Wake. Wala msirudi nyuma kwenye viapo mlivyovitilia mkazo, na hali mlimfanya Allah Mtukufu Ndiye mdhamini na msimamizi mlipomuahidi. Hakika Allah Mtukufu Anayajua mnayoyafanya na Atawalipa kwayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net