Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 90

An-Nahl 16:90

النحل

إِنَّ ٱللَّهَ يَأْمُرُ بِٱلْعَدْلِ وَٱلْإِحْسَـٰنِ وَإِيتَآئِ ذِى ٱلْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ ٱلْفَحْشَآءِ وَٱلْمُنكَرِ وَٱلْبَغْىِ ۚ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa, na anakataza uchafu, na uovu, na dhuluma. Anawaaidhi ili mpate kukumbuka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani,na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka. [90]

[90] Mwenyezi Mungu anawaamrisha waja wake uadilifu wa maneno na vitendo, na katika kila jambo wakusudie lilio bora, na walifadhilishe kuliko jenginelo. Kama anavyo amrisha kuwapa jamaa zenu wanacho hitajia, ili kuzidi kutia nguvu makhusiano ya mapenzi kati ya ukoo. Na Mwenyezi Mungu anakataza kutenda kila la makosa, na khasa madhambi yaliyo pita mpaka kwa ubaya, na kila kisicho pendeza katika sharia na akili nzuri. Hali kadhaalika anakataza kumfanyia uadui mtu. Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika anakukumbusheni haya, na anakuelekezeni kwenye mambo mema, mpate kukumbuka fadhila zake kwa maelekezo yake mema,basi ndio mfanye anavyo kwambieni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Anawaamrisha waja Wake ndani ya Qur’ani hii wawe waadilifu, wafanye usawa katika kutunza haki Yake, kwa kumpwekesha Yeye na kutomshirikisha, na haki ya waja Wake, kwa kumpa haki yake kila mwenye haki. Na Anaamrisha kufanya wema katika kutekeleza haki Yake, kwa kumuabudu na kutekeleza faradhi Zake kwa namna ilivyopasishwa na Sheria, na kuwafanyia wema viumbe Wake katika maneno na vitendo. Na Anaamrisha kuwapa walio na ukaribu wa ujamaa kitu cha kuwaunga na kuwatendea wema. Na Anakataza kila ambalo ni ovu, likiwa ni neno au ni tendo, na ambalo Sheria inalipinga na haikubaliani nalo la ukafiri na maasia, na kuwadhulumu watu na kuwafanyia maonevu. Na Allah Mtukufu, kwa maamrisho haya na makatazo haya, anawapa mawaidha na kuwakumbusha mwisho mbaya, ili mzikumbuke amri za Allah Mtukufu na mnufaike nazo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net