Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 89

An-Nahl 16:89

النحل

وَيَوْمَ نَبْعَثُ فِى كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا عَلَيْهِم مِّنْ أَنفُسِهِمْ ۖ وَجِئْنَا بِكَ شَهِيدًا عَلَىٰ هَـٰٓؤُلَآءِ ۚ وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ ٱلْكِتَـٰبَ تِبْيَـٰنًا لِّكُلِّ شَىْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ

Maana

Na (waonye) siku tutakapomtoa shahidi katika kila umma kutokana na wao wenyewe, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hawa. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu, na ni uongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na (waonye) siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa yanayo tokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu,na rehema, na bishara kwa Waislamu. [89]

[89] Ewe Nabii! Wahadharishe makafiri katika kaumu yako kwa yatakayo wapata Siku tutapo watolea kila umma shahidi wa kuwashuhudia, naye ndiye Nabii wao, ambaye atakuwa ni mmoja wao, ili wawe hawana kisingizio. Na wewe, ewe Nabii, tutakuleta uwashuhudie hao walio kukadhibisha. Na tangu hivi sasa yawapasa wazingatie! Sisi tumekuteremshia wewe Qur'ani, ambayo ndani yake kila kitu kimebainishwa kwa haki. Na ndani yake umo uwongofu, na rehema, na bishara ya Pepo kwa wenye kuifuata na kuiamini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka, ewe Mtume, pindi tutakapomleta, Siku ya Kiyama, katika kila ummah miongoni mwa ummah zote, shahidi juu yao: naye ni Mtume ambaye Allah Mtukufu Alimpeleka kwao anayetokana na wao wenyewe na kwa lugha yao, na tukakuleta wewe, ewe Mtume, ukiwa ni shahidi juu ya ummah wako. Na kwa kweli, tumekuteremshia Qur’ani ikiwa na ufafanuzi wa kila jambo linalohitajia maelezo, kama hukumu za halali na haramu, malipo mema na mateso na yasiyokuwa hayo, na ili iwe ni uongofu wenye kutoa kwenye upotevu, na ni rehema kwa atakayeiamini na kuifuata kivitendo, na iwe ni bishara njema kwa Waumini kwamba watakuwa na mwisho mwema.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net