An-Nahl 16:88
النحلٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَصَدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ زِدْنَـٰهُمْ عَذَابًا فَوْقَ ٱلْعَذَابِ بِمَا كَانُوا۟ يُفْسِدُونَ
Wale waliokufuru na kuzuilia njia ya Mwenyezi Mungu, tutawazidishia adhabu juu ya adhabu, kwa walivyokuwa wakifanya uharibifu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wale walio kufuru na kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu tutawazidishia adhabu juu ya adhabu, kwa walivyo kuwa wakifisidi. [88]
[88] Walio kufuru na wakawazuia wengine kufuata Njia ya Mwenyezi Mungu, nayo ndiyo Njia ya kheri na haki, tutawazidishia adhabu juu ya adhabu wanayo stahiki kwa ukafiri wao, kwa walivyo kusudia kuwafisidi na kuwapotosha waja wa Mwenyezi Mungu!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wale ambao waliukanusha upweke wa Allah Mtukufu na unabii wako, ewe mtume, na wakakukanusha wewe, wakawakataza wengine wasimuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, tutawazidishia adhabu juu ya ukanushaji wao na adhabu juu ya kuwazuia watu kuifuata haki. Na hili ni kwa sababu ya kukusudia kwao kufanya uharibifu na kuwapoteza waja kwa ukafiri na uasi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net