Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 92

An-Nahl 16:92

النحل

وَلَا تَكُونُوا۟ كَٱلَّتِى نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِنۢ بَعْدِ قُوَّةٍ أَنكَـٰثًا تَتَّخِذُونَ أَيْمَـٰنَكُمْ دَخَلًۢا بَيْنَكُمْ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِىَ أَرْبَىٰ مِنْ أُمَّةٍ ۚ إِنَّمَا يَبْلُوكُمُ ٱللَّهُ بِهِۦ ۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ مَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ

Maana

Wala msiwe kama mwanamke yule aliyeufumua uzi wake baada ya kwishausokota ukawa mgumu. Mnavifanya viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu kwa kuwa ati umma mmoja una nguvu zaidi kuliko mwingine? Hakika Mwenyezi Mungu anawajaribu kwa njia hiyo. Na bila ya shaka atawabainishia Siku ya Kiyama yale mliyokuwa mkihitilafiana ndani yake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala msiwe kama mwanamke anaye uzongoa uzi wake baada ya kwisha usokota ukawa mgumu. Mnavifanya viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu kwa kuwa ati taifa moja lina nguvu zaidi kuliko jengine? Hakika Mwenyezi Mungu anakujaribuni kwa njia hiyo. Na bila ya shaka atakubainishieni Siku ya Kiyama mliyo kuwa mkikhitalifiana. [92]

[92] Wala msiwe katika kwenda kinyume na viapo vyenu baada ya kuvithibitisha mfano wa mwanamke mwendawazimu anaye sokoto sufi, ikisha kuwa nyuzi akazifumua tena. Mkafanya viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganya na kukhadaa watu, na huku mkijitafutia udhuru kwa kuwa ama nyinyi ni wengi zaidi au mna nguvu zaidi kuliko wao, au mnakusudia kuwaunga mkono maadui wenye nguvu zaidi kuliko wao, au kwa kuwa mnataraji kuzidi nguvu kwa khiana! Na hakika Mwenyezi Mungu anakufanyieni mtihani. Mkikhiari kutimiza ahadi mtapata mavuno ya duniani na Akhera. Mkielekea khiana, basi ni khasara yenu. Na hakika Siku ya Kiyama atakubainishieni ukweli wa khitilafu zenu za duniani, na atakulipeni kwa mujibu wa vitendo vyenu. Aya mbili hizi zinaonyesha kuwa msingi wa makhusiano baina ya Waislamu na wengineo pamoja na uadilifu ni kutimiza ahadi, na kwamba makhusiano baina ya mataifa hayasimami sawa ila kwa kutimiza ahadi, na kwamba dola za Kiislamu zikijifunga kwa mapatano basi zijifunge kwa jina la Mwenyezi Mungu. Maana ya hayo ni kuwa inakuwapo yamini ya Mwenyezi Mungu na kuwa Yeye ndiye dhamini. Na Aya inafahamisha mambo matatu, ambayo lau kuwa mataifa yangeli yatimiza basi amani ingeli enea: Kwanza: Haifai mapatano kuwa ndio njia ya kufanya khadaa. Ikiwa hivyo inakuwa ni udanganyifu. Na udanganyifu haufai katika makhusiano baina ya wanaadamu, sawa sawa ikiwa baina ya mtu na mtu, au kikundi na kikundi, au baina ya madola. Pili: Kutimiza ahadi peke yake ni nguvu. Na mwenye kuvunja ahadi ni kama mwenye kuvunja alicho kijenga kwa sababu za nguvu. Basi anakuwa kama mpumbavu anaye tatua uzi wake kila akisha usokota. Tatu: Haimfalii mtu kuvunja ahadi kwa sababu ya kutafuta nguvu au kutaka kuzidisha kipande cha ardhi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wala msirudi nyuma kwenye ahadi zenu, ukawa mfano wenu ni kama wa mwanamke aliyefuma mfumo akautengeneza vizuri kisha akaufumua, Mnavifanya viapo vyenu mlivyoviapa wakati wa makubaliano kuwa ni udanganyifu kwa mliyopatana naye, mkawa mnazivunja ahadi zenu mnapopata kundi la watu wenye mali kuliko wale mlioahidiana nao. Kwa hakika, Allah Mtukufu Anawapa mtihani kwa kuwaamrisha nyinyi mtekeleze ahadi na kuwakataza nyinyi msizivunje. Na ili Apate kuwaeleza, Siku ya Kiyama, yale ambayo mlikuwa mkitofautiana kwayo kuhusu kumuamini Allah Mtukufu na kuuamini unabii wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net