Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 93

An-Nahl 16:93

النحل

وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَٰحِدَةً وَلَـٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهْدِى مَن يَشَآءُ ۚ وَلَتُسْـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Maana

Na Mwenyezi Mungu angelitaka, kwa yakini angeliwafanya kuwa umma mmoja. Lakini anampoteza amtakaye, na anamwongoa amtakaye. Na hakika mtaulizwa juu ya yale mliyokuwa mkiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu angeli taka, kwa yakini angeli kufanyeni umma mmoja. Lakini anamwachia kupotea anaye mtaka, na anamwongoa amtakaye. Na hakika mtaulizwa kwa yale mliyo kuwa mkiyafanya. [93]

[93] Mwenyezi Mungu ange taka angeli kufanyeni nyote umma wa namna moja kwa jinsi, na rangi, na imani, bila ya khitilafu. Na hayo ni kwa kukupeni umbo jengine, mkawa kama Malaika wasio na uwezo wa kukhiari watakalo. Lakini ametaka muwe jinsi na rangi mbali mbali, na akakupeni uwezo wa kukhiari wenyewe. Mwenye kukhiari matamanio ya dunia kuliko kumridhi Mwenyezi Mungu, anaachwa kwa ayatakayo. Na mwenye kutaka kumridhi Mwenyezi Mungu kwa vitendo vyema, anasahilishiwa kwa anayo yataka. Na kuweni na yakini kuwa nyote nyinyi mtakuja ulizwa Siku ya Kiyama juu ya mliyo yatenda duniani, na mtalipwa kwa vitendo vyenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau Allah Mtukufu angalitaka angaliwaafikia nyote Akawafanya muwe kwenye muelekeo mmoja, nao ni Uislamu na Imani, na Angaliwalazimisha nao. Lakini Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Anampoteza Anayemtaka, kati ya wale ambao Yeye Alijua kuwa walichagua upotevu, Asimuongoze kwa uadilifu Wake. Na Anamuongoza Anayemtaka, kati ya wale ambao Yeye Alijua kuwa wao walichagua haki, Akampa muelekeo kwa wema Wake. Na Allah Mtukufu Atawauliza nyinyi nyote, Siku ya Kiyama, yale ambayo mlikuwa mkiyafanya ulimwenguni kati ya yale Aliyowaamrisha nayo na Aliyowakataza, na Atawalipa nyinyi kwa hayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net